Tanesco

Utilities

Umeme Park, Ubungo, Dar es Salaam

www.tanesco.co.tz/

Do you manage this business/place? Claim it here

Total ratings: 0

Average rating

Total reviews: 1

Write a review
Others' reviews
TANESCO; hili ndilo shirika uozo kuwahi kutokea kwa upande wangu. Kitu ambacho mnakifanya kwa ufanisii mkubwa zaidi na hapo ninyi ni bora duniani kote ni kukata umeme, sasa nashindwa kuelewa uwepo wenu unamaana gani? Mvua ikinyesha dakika 5 tu kisingizio tosha, kila siku wakurugenzi wanasimamishwa na kufukuzwa kabisa lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya hapo na serikali yenu inakaa kimya au inawa tetea tu. Sioni sababu kwanini monopoly iendelee kwenye hii sekta, kwanini usiongezwe ushindani kwa kuruhusu wanaoweza kuzalisha umeme kwa ufanisi wa ugawaji wa umeme na si kwa ukataji umeme? Eti tukiruhusu ushindani tutaliua hili shirika inabidi tuliimarishe kwanza ndipo turuhusu ushindani; hoja gani hii isiyobeba maji hata lita moja tu kwa taifa linalotakiwa kukimbia kuelekea kunako maendeleo? Kwani tanesco ni baba au mama yetu kwamba akifa tumepoteza mzazi tena muhimu kiasi hicho? Yapo wapi mashirika mengine ya umma ambayo yalikuwapo kabla na hata baada ya tanesco? Ilikuwaje yalikufa kama si kwa upuuzi wao na wizi uliokithiri? Vipi baada ya vifo vya hayo mashirika Tanzania nayo imekufa au imenawiri zaidi? Yawezekana yangekuwapo tungekuwa mbali zaidi ya tulipo, pia yawezekana tungekuwa nyuma zaidi ya tulipo na hili ndilo naliamini zaidi sababu sisi watanzania kila nafasi tunayopata tunawaza zaidi matumbo yetu na familia zetu kuliko tumbo kubwa ambalo ndio hii nchi yetu. Miaka imepita mingi sana tangu serikali ianze maneno ya kuiimarisha tanesco, ajabu hasara zinazidi tu kutokea ndani ya shirika, wakurugenzi wanendela kusimamishwa kupisha uchunguzi na hatimaye kufukuzwa, nadhani ndicho tunachoweza maana hata mimi nikiingia nitakula nikijua; baada ya kukamatwa nitasimamishwa halafu nitafukuzwa wakati huo nimesha kula sana halafu hakuna litakaloendela. Nitakuwa na pesa za kutosha katika benki kula miaka ishirini mbele, nani anajali? Alipongia waziri mpya, uteuzi uliopita wa muheshimiwa Raisi Jakaya aliahidi mgao kuwa historia. Kinacchotokea sasa hivi ni zaidi ya mgao, tanesco wamekuwa wafanisi sana kwenye kukata umeme sabau marekebisho ambayo hayaishi. Juzi; jumatatu 12/11/2012 umeme ulikatika kwa masaa ya kutosha sana, nchi iliingia kwenye giza kali sana. Majira ya saa moja jioni dar es salaam ilikuwa giza totorooo, arusha hivyo hivyo si ajabu hata mwanza mambo yalikuwa yaleyale. Nikajiuliza kama hali hii inatokea tukiwa na baraza la mawazi kubwa hivi vipi tungekuwa na mawaziri ishirini tu? Nadhani nchi ingekuwa gizani mwezi mzima. Ninachojiuliza kwasasa, hivi ushindani ukiruhusiwa makampuni yakaongezeka katika kuzalisha umeme nchi itakuwa kwenye upande wa hasara au faida? Hasara kubwa kwa taifa ni ipi; tanesco ife na umeme uzalishwe? Au tanesco iendelee na ufanisi wake katika kukata umeme na nchi izidi kurudi nyuma kimaendeleo? Sababu naamini umeme unachukua sehemu kubwa sana ya maendeleo hasa katika hii dunia ya teknologia ya sayansi. Sidhani kama huu ni uamuzi mgumu hata kidogo, watu waachane na kuendekeza interest binafsi na kuliacha taifa. Yapo mengi sana hata wewe unayajua laini utakaposema nani atajali? Ukiwa peke yako darasani utaendelea kushika nafasi ya kwanza tu hatutajali wastani wako na hakutakuwa na kipimo kwa kukupima uwezo wako, ushindani ni muhimu. SIIPENDI TANESCO NA NADHANI INASTAHILI KUZIKWA!

How would you rate this review?

Helpful 0
Funny 0
Awesome 0